Machoni kama watu - Museke African song lyrics

Tagged:  •    •    •    •    •  
  • Machoni kama watu
    Enable Javascript and
    Adobe Flash player in your browser to browse the full media gallery

    View all from A-Y
    Raha Kamili
    A-Y, Lady Jaydee
    Swahili
    3:35
    1
    Ambwene Allen Yessayah
    2003

Chorus
Machoni kama watu
Mioyoni hawana utu
Imani imetoweka
Mabaya yanaongezeka

Verse 1
Wengi wao wanatabasamu, wanaongea kwa nidhamu
Wanajifanya watu wa karib kumbe hao ndo sumu
Wameweka mbele dini fungo moyo usiwaamini
(Si unakumbuka alikufaa kwa dhiki)
Kweli
(Enzi zile upo nae marafiki)
Aha, yuko wapi sasa hayupo tena ashasaliti
Kweli akufaae kwa dhiki mara nyingine ni msaliti
Alishatembea na mkeo kwa gia ya urafiki
Shoga yako kwako habanduki mmeo akakutaliki
Unajuta ye anacheka kwani ndoa keshaivuruga
Mmeo ametimua ye keshatawala nyumba
Baba na nyumba ndogo watoto wanalia mateso
Anadiriki hata kuwakana hana huruma hata kidogo
Haina mshangao watu wa aina hii wapo
Sio sehem zingine hata hapa ulipo wapo
Jirani yako mchana mnacheka usiku mwanga
Nia yake kuona life oh inapinda
Dili zote zigime mipango igonge mwamba afya yako
Bandika bandua ya magonjwa itatamba......

Repeat Chorus

Verse 2
Yoh! dunia inavunda vvu walimwengu hawashikiki
Wengi wanapenda ngono lakini kuzaa hawataki
Wengi nacheka nao tu lakini sio kwa dhati
Hivyo ni kama nipo gizani halafu nalamba ncha ya mkuki
Wengi wanatoa mimba wengine wanatupa watoto
Ungekuwa wapi mama yako angekutupa enzi hizo
Imani hakuna ndani ya maovu yasio na mwisho
Nakata tamaa akili inachoka moyo mzito
Machoni kama watu kumbe wamejaa unyama tu
Kaa chonjo chunga sana napo akili kichwani tu
Hapendi kukuona unatesa juu yako mzigo chuki
Ameshatega mabaya mitego ndo haikamatiki
Hapendi kuona unawini hapendi kuona unafuraha
Raha yake kuona umezungukwa na karaha
Hana raha anapoona mambo safi kiuchumi
Moyo utakuwa shwari tu pale una hali duni

Repeat Chorus

Verse 3
Huyo ndo mwanadamu anapowini tu dharau
Napo ni mgumu kuelewa mwepesi kusahau
Anajionyesha ana huruma,mpole na mkarimu
Na aliye mstari wa mbele kutoa ahadi tamu
Usimpa nafasi hata ajue zako habari
Hana jema chunga sana hana ujio wa heri
Hataki kabisa kuona unavuta hewa hii lakini
Wapi mipango inabaki zzzzz!!
Ni rahisi kwake kupata mali kwa njia ya kuua
Haya mambo hi hali nadhamni wote mnaijua
Mlale pema mliouwawa mkidai zenu haki
Sisi bado tupo duniani hatujui lini tamati
Jasho la mnyonge huwa ni neema kwa wachache
Ni kilio cha fukara chenye lengo haki nipate
Stuka huko tunakokwenda kunatisha
Kwani itakuwa ndoto watu kutenda mema kabisa

© A-Y

Related
Museke African song lyricsUsijaribu (Mikono juu)1, Yule2, Binadamu3, Shake it6, Go back to her7, Story of my life8, Kom speel9, Falling in love10, Umunt'onjani lo12, Dali Wami (Ntando)13, Mngani Wam14, Nabikoowa15, Kibaluma16, Tamika17, Leah18, Afrique19, Zali la mentali21, Poa22, Ndawo yami (my place)23, Sogea sogea25, Sikuhitaji26, Katupakase (tukole)27, Sivyo Ndivyo28, Emlanjeni29, Ndihamba Nawe30, O tswa kae 31, Ma'cheri32, Maisha (my life)33, Sinzia34, Black President35, Phezulu36, High I go37, Sondela38, Riziki39, Everytime41, Butterflies42, Everyone's Child 43, Wandirasa 44, Siku hazigandi47, Wanaume kama mabinti48, Distance49, Mhla'uphel'amandla 50, Baby Tonight52, Cinderella (Ali Kiba)54, What's hardcore56, Hoobale57, Never Change My Mind 58, The Superstar60, Gimme love61, Kenyan gal, Kenyan boy62, Fire anthem63, Chochote utapata64, Ninanoki65, Fiasco66, Sekunjalo67, Nchi ya kitu kidogo68, Lwandle 70, Siwema71, Twende Twende 72, Bless ma room73, African dream74, Click Song (Qongqothwane)75, Pink confetti76, Wa tuba tuba 77, Tsho Tsho79, Dubula, dubula, dubula80, Karolina81, Subhaa82, Cape to Cairo84, Vumile85, Niwe wako88, Bembeleza89, Motherland (Tribute to Africa)90, Jamila91, Mama Rhoda92, International93, Dunia mapito94, Kuna dawa95, Liar96, Wailai98, Ngaphesheya 99, Karibia101, World of scandals102, Crazy party103, Music & Lights104, Feel good106, Quadradinha107, Nita Mukuma Kwini109, I love you (Yola)110, I'm burning up111
Museke African artistesA-Y4, Gal Level11, Professor Jay20, Tumi and the Volume24, Jamnazi Africa40, Chiwoniso45, Malaika46, Lady Jaydee51, Alikiba53, Zola55, Juliana Kanyomozi59, Eric Wainaina69, Koldproduk78, Kabelo83, Zamajobe Sithole86, Nikki87, Wahu97, Top in Dar (TID)100, Matonya105, Yola Araujo108
Museke African mixes/playlistsAfro-ES5

Post new comment

The content of this field is kept private and will not be shown publicly.
  • Enclose a word in <d> tags to link to a dictionary search
  • Enclose a word in <m> tags to link to a Museke search
  • Enclose a word in <s> tags to link to a search on this website
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Youtube and Google video links are automatically converted into embedded videos.

More information about formatting options