Vijimambo - Museke African song lyrics

Tagged:  •    •    •    •    •  
  • Vijimambo
    Enable Javascript and
    Adobe Flash player in your browser to browse the full media gallery

    View all from Noorah
    Vijimambo
    Noorah
    Swahili
    http://www.youtube.com/watch?v=YWmyFr_REAo
    Noorah
    2007

Intro
Hivi nani..........Hivi nanii vijimambo

Chorus
Usishangae usione hatari (vijimamabo)
vipo hivi kila siku (vijimambo)
mjomba wewe vimekukuta? (vijimambo)
hivi nani...............vijimambo

Verse 1
Si muda mrefu sana toka nimalize shule/
bado nahangaika mambo yangu yatulie/
kula kulala kwa baba kuwa napenda/
ni vile mtandao bora wa maisha sijaujenga/
(anyway) mtaani kuna binti kanichengua/
na kwa utajiri wangu wa sera wimbo atautambua/
Uwaridi u mzima? muungwana naomba faragha/
ninene maanani yale yatakayokupa faraja/
yarabi toba, mtoto akapanga tarehe/
tukutane bar moja iitwayo starehe/
haya zikaanza resi huku na huku/
kusaka mshiko madem zao si chips kuku/
cha ajabu mpaka siku ya siku/
dili zimejamba najikuta mfukoni nna buku/
hamna noma dem mwenyewe sister duu/
tutaenda bar ye na Fanta mengine juu kwa juu/
nisivyotarajia si akaagiza heineken/
mzee mzima mmh! nikaona hiki kibembe/
miti huteleza nyani aelekeapo kufa/
heineken tatu sasa binti ameshazifuta/
mrembo akazama msalani
shetani langu likanituma ndani ya pochi yake mezani/
pap! buku buku sambamba na blue bleu/
nahitaji buku mbili ku-solve mtihani huu/
nshazikamata naa nishaanza kuzivuta/
nagongwa bega nani! ,mwenyewe amenikuta/
unafanya nini kwenye pochi yangu?
Aaa mmh aaa mmh mmmh mmmh!

Chorus 2x

Verse 2
Napiga nondo najaa nshajiamini/
wiki tatu gym Tyson ndio mimi/
popote penye zali ukija utaniona mimi/
nakugonga ukiuliza najibu utafanya nini?
siku nyingine kijambo kingine/
ndai ya hiace naenda town mida saa 4/
ndani ya seat level na madenti wawili bomba/
abiria tuko kimya konda tu anachonga/
mara akawanza madent na kauli zake mbovu/
nikimcheki konda mwenyewe namuona mchovu/
japo madenti wenyewe siwajui/
nikanunua kesi mradi nikombe uspuni/
ikaanza vita ya maneno mi na konda/
nikinya mbovu ye ahara akipaka nnaponda/
akanizidi kuchonga/
kuvumilia no! kimabavu nkatishia kumbonda/
bila ubishi konda bodi akagonga/
ngoma kushoto kilichofuata nauli kulipa/
kuji search sindo nikakumbuka/
pesa yote iko nyumbani kwenye jeans niliyoibadilisha/aah
oyaa lete nauli hiyo!!

Chorus 2x

Verse 3
Misosi ya uswazi huwa imenuna/
ni mboga moja iwe na wali au nguna/
kama ni tunda ndizi tena moja sunasuna/
ni kula usife alimradi siku kuisukuma/
demu kaniita lunch sinza/
nikikataa nitamliza/
kwahiyo ikabidi nifunge safari sinza/
kufika napewa juice sijui ya nini?/
acha hii ya passion tuliyozoea uswahilini/
nikapiga glasi ya kwanza na kuongeza ya pili/
kila sekunde chache mzee napiga funda 2
nikaitwa mezani ooh boy menu si ya kitoto/
ubwabwa wa rangi mikukukuku pocho pocho/
sikuacha kitu vyote nikagusa/
baada ya kula jifuta mambo si yakageuka!/
tumbo kuunguruma utadhani limeshtuka/
nikaomba nionyeshweuwani kabla hayajashuka/
noma zaidi ni pale nilipoinuka/
nikajua sasa hivi wa tafrija naumbuka/
kufika toi kabla mlago sijafungua/
trouser mapajani mara ngoma ikafumuka/
chafua sink eneo lote lililonizunguka/
kucheki maji ooh yamekatika/
kabla sijajua muda niliotumia chooni/
mara vibaya nasikia mtu anagonga mlangoni/
Mh mwanangu hujamaliza na mimi nataka kuingia/
oooo hoooo!!!!

Chorus 2x

Outro
hallow/ahaa Saddam Hussein/assalam alaikum,
eeh sasa we rafiki yangu unanipigia sim sasa hivi mi niko studio narekodi!
eeh fanya hivi we nipigie kama baada ya dakika 10 hivi/
eeh au ni beep halafu mi nitakupigia/
msalimie TAREK AZIZ

© Noorah

:

Watch the Vijimambo video by Noorah:

Post new comment

The content of this field is kept private and will not be shown publicly.
  • Enclose a word in <d> tags to link to a dictionary search
  • Enclose a word in <m> tags to link to a Museke search
  • Enclose a word in <s> tags to link to a search on this website
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Youtube and Google video links are automatically converted into embedded videos.

More information about formatting options